Man city yapeleka msiba tena kwa mashabiki wa arsenal

Ni baada ya ushindi mwingine zidi ya arsenal meneja wa manchester city, Pep Guardiola afunguka na kusema wapo karibu na ubingwa.

Manchester city yaendeleza ubabe dhidi ya arsenal katika uwanja wa Emirates baada ya kuinyuka magoli 3 kwa 0. Bernardo silva ndiye alikuwa wa kwanza kupeleka msiba huo kwa timu ya arsenal baada ya kufunga goli katika dakika ya 15 ya mchezo, lakini katika dakika ya 28 ya mchezo David silva aliifungia timu yake goli la pili na dakika tano baadae mchezaji Leroy Sane alifunga goli la tatu. Arsenal walipata nafasi ya kufunga goli la kufutia machozi baada kupata penati, lakini uimara wa mlinda mlango wa man city  Ederson kucheza penati iliyopigwa na Pierre-Emerick Aubameyang na kuwafanya arsenal kutoka patupu.
Kwa matokeo hayo Manchester city anahitaji kushinda mechi tano kati ya kumi zilizobaki ili aweze kutangaza ubingwa huku Arsenal wenyewe wakizidi kujiweka pabaya kwenye mbio za kuwania top four ili kuwawezesha kushiriki UEFA kwa msimu unaokuja.

By David peter

Comments

Popular posts from this blog

Manchester united win 2-1 over chelsea

TCRA yafungia nyimbo za wasanii zisizo na maudhui mazuri ya kitanzania

Idadi ya wafungwa Tanzania kuzidi uwezo wa magereza