Posts

Showing posts from March, 2018
Image
Msanii wa hip hop na rapa wa Tanzania Roma Mkatoriki akumbana na adhabu ya kutotoa kazi yoyote ya muziki na kutoshiriki tamasha wala show yoyote kwa muda wa miezi sita  kutoka kwenye balaza la  wasanii Tanzania BASATA baada ya kutoitikia mwito wa kikao na BASATA. “Huyu ndugu anayeitwa Roma Mkatoliki tunampa adhabu, kwa mujibu wa katiba na kanuni ambazo zinatuongoza sisi. kwa hiyo tunamfungia kwa miezi sita. Ndani ya hiyo miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote wa sanaa, hakuna kuperform kwenye tamasha lolote, na wimbo huo moja kwa moja tunaufungia,” amesema Naibu Waziri, Juliana Shonza. Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi,, Machi 1, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameeleza kuwa msanii huyo amewahi kupewa onyo la kubadilisha jina la wimbo huo pamoja na baadhi ya maneno yaliyomo ndani yake, lakini alikaidi na wimbo huo ukaendelea kupigwa katika vyombo mbalimbali vya habari. Shonza ameongez...

TCRA yafungia nyimbo za wasanii zisizo na maudhui mazuri ya kitanzania

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepokea orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Nyimbo hizo zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii. Kutokana na nyimbo hizo kuwa na maudhui ambayo ni kinyume na kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005, mamlaka hiyo imeviagiza vyombo vya habari kusitisha nyimbo hizo. Orodha ya nyimbo hizo ni kama ifuatavyo:- 1. Hallelujah – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz 2. Waka waka – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz 3. Kibamia – Aberdnego Damian a.k.a Roma Mkatoliki 4. Pale Kati Patamu – Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego 5. Hainaga Ushemeji – Amani Hamisi a.k.a Manifongo 6. 6I am Sorry JK – Nicas John Mchuche a.k.a Nikki Mbishi 7. Chura – Snura Mushi a.k.a Snura 8. Tema mate tumchape – Hamad Ali a.k.a Madee 9. Uzuri Wako – Juma Musa Mpolopoto a.k.a Jux 10. Nampa Papa – Gift Stanford a.k.a Gigi Money 11. Nampaga – Barnaba Elias a....

Man city yapeleka msiba tena kwa mashabiki wa arsenal

Image
Ni baada ya ushindi mwingine zidi ya arsenal meneja wa manchester city, Pep Guardiola afunguka na kusema wapo karibu na ubingwa. Manchester city yaendeleza ubabe dhidi ya arsenal katika uwanja wa Emirates baada ya kuinyuka magoli 3 kwa 0. Bernardo silva ndiye alikuwa wa kwanza kupeleka msiba huo kwa timu ya arsenal baada ya kufunga goli katika dakika ya 15 ya mchezo, lakini katika dakika ya 28 ya mchezo David silva aliifungia timu yake goli la pili na dakika tano baadae mchezaji Leroy Sane alifunga goli la tatu. Arsenal walipata nafasi ya kufunga goli la kufutia machozi baada kupata penati, lakini uimara wa mlinda mlango wa man city  Ederson kucheza penati iliyopigwa na Pierre-Emerick Aubameyang na kuwafanya arsenal kutoka patupu. Kwa matokeo hayo Manchester city anahitaji kushinda mechi tano kati ya kumi zilizobaki ili aweze kutangaza ubingwa huku Arsenal wenyewe wakizidi kujiweka pabaya kwenye mbio za kuwania top four ili kuwawezesha kushiriki UEFA kwa msimu unaokuja. By D...