Posts

Showing posts from 2018
Image
Mamia ya wanawake waliotelekezwa baada ya kuzalishwa na waume zao wamejazana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyetangaza kuanza kuwasikiliza. Kumekuwa na mafuriko ya wanawake wanaoingia kwa kusukumana kwenye ofisi hizo hali iliyowalazimu walinzi kufunga geti ili walio ndani wahudumiwe. Wanasheria na wafanyakazi wengine wa ofisi hiyo wanaendelea kuwasikiliza wanawake hao wengi wao wakiwa wamebeba watoto wao. Wakizungumza na MCL Digital leo, Aprili 9 wanawake hao wamesema wingi wao unaweza kusababisha baadhi yao kushindwa kusikilizwa. "Nilitelekezwa na watoto wanne kwenye nyumba ya kupanga, nimekuwa kama ombaomba nashukuru Makonda ameona kilio chetu lakini kwa umati huu naogopa sana,"amesema mwanamke mmoja. Wapo waliolala kwenye ofisi hizo huku wengine wakianza kuwasili tangu saa tisa za usiku.  Vimetengwa vyumba maalum zikiwamo kumbi zilizo katika ofisi hizo kwa ajili ya kusikiliza kilichowasibu wanawake hao.

Idadi ya wafungwa Tanzania kuzidi uwezo wa magereza

Image
Tanzania inakadiriwa kuwa na wafungwa 40,000 wakati uwezo wa magereza yake ni 30,000 hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 katika msongamano huo. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Hamad Yusufu Masauni wakati akijibu swali la nyongeza la Ruth Mollel ambaye ametaka kujua Serikali inafanya nini kumaliza msongamano wa wafungwa. Masauni amesema kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 ambapo kwa sasa Serikali inafanya kila namna kumaliza msongamano huo. Katika swali la msingi Mwantakaje  Haji Juma  (BUBUBU-CCM) amehoji ni lini kituo cha polisi katika jimbo lake kitafanyiwa ukarabati. Naibu Waziri amesema kituo hicho kitafanyiwa kazi wakati wowote fedha ikipatikana ili kiwawezeshe askari kutoa huduma bora.
Image
Msanii wa hip hop na rapa wa Tanzania Roma Mkatoriki akumbana na adhabu ya kutotoa kazi yoyote ya muziki na kutoshiriki tamasha wala show yoyote kwa muda wa miezi sita  kutoka kwenye balaza la  wasanii Tanzania BASATA baada ya kutoitikia mwito wa kikao na BASATA. “Huyu ndugu anayeitwa Roma Mkatoliki tunampa adhabu, kwa mujibu wa katiba na kanuni ambazo zinatuongoza sisi. kwa hiyo tunamfungia kwa miezi sita. Ndani ya hiyo miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote wa sanaa, hakuna kuperform kwenye tamasha lolote, na wimbo huo moja kwa moja tunaufungia,” amesema Naibu Waziri, Juliana Shonza. Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi,, Machi 1, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameeleza kuwa msanii huyo amewahi kupewa onyo la kubadilisha jina la wimbo huo pamoja na baadhi ya maneno yaliyomo ndani yake, lakini alikaidi na wimbo huo ukaendelea kupigwa katika vyombo mbalimbali vya habari. Shonza ameongez...

TCRA yafungia nyimbo za wasanii zisizo na maudhui mazuri ya kitanzania

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepokea orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Nyimbo hizo zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii. Kutokana na nyimbo hizo kuwa na maudhui ambayo ni kinyume na kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005, mamlaka hiyo imeviagiza vyombo vya habari kusitisha nyimbo hizo. Orodha ya nyimbo hizo ni kama ifuatavyo:- 1. Hallelujah – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz 2. Waka waka – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz 3. Kibamia – Aberdnego Damian a.k.a Roma Mkatoliki 4. Pale Kati Patamu – Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego 5. Hainaga Ushemeji – Amani Hamisi a.k.a Manifongo 6. 6I am Sorry JK – Nicas John Mchuche a.k.a Nikki Mbishi 7. Chura – Snura Mushi a.k.a Snura 8. Tema mate tumchape – Hamad Ali a.k.a Madee 9. Uzuri Wako – Juma Musa Mpolopoto a.k.a Jux 10. Nampa Papa – Gift Stanford a.k.a Gigi Money 11. Nampaga – Barnaba Elias a....

Man city yapeleka msiba tena kwa mashabiki wa arsenal

Image
Ni baada ya ushindi mwingine zidi ya arsenal meneja wa manchester city, Pep Guardiola afunguka na kusema wapo karibu na ubingwa. Manchester city yaendeleza ubabe dhidi ya arsenal katika uwanja wa Emirates baada ya kuinyuka magoli 3 kwa 0. Bernardo silva ndiye alikuwa wa kwanza kupeleka msiba huo kwa timu ya arsenal baada ya kufunga goli katika dakika ya 15 ya mchezo, lakini katika dakika ya 28 ya mchezo David silva aliifungia timu yake goli la pili na dakika tano baadae mchezaji Leroy Sane alifunga goli la tatu. Arsenal walipata nafasi ya kufunga goli la kufutia machozi baada kupata penati, lakini uimara wa mlinda mlango wa man city  Ederson kucheza penati iliyopigwa na Pierre-Emerick Aubameyang na kuwafanya arsenal kutoka patupu. Kwa matokeo hayo Manchester city anahitaji kushinda mechi tano kati ya kumi zilizobaki ili aweze kutangaza ubingwa huku Arsenal wenyewe wakizidi kujiweka pabaya kwenye mbio za kuwania top four ili kuwawezesha kushiriki UEFA kwa msimu unaokuja. By D...

DC wa Shinyanga aendesha oparesheni ya mazingira na usafi

Image
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendesha oparesheni ya usafi na Mazingira kukagua usafi na miti iliyotelekezwa na kuwawajibisha wananchi ambao miti yao imekufa kwa kulipa faini ya shilingi 50,000/= kwa kila mti na kuwataka wapande miti mingine.  Mkuu huyo wa wilaya amefanya oparesheni hiyo Februari 24,2018 katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga ambapo kila mwananchi ambaye miti iliyopandwa kwenye eneo lake imekufa aliwajibishwa kwa kufanya uzembe na kusababisha miti ife.  Katika opareshini hiyo kila mwananchi aliyepigwa faini alikuwa anapatiwa risiti ya malipo na aliyeshindwa kulipa alikuwa anapandishwa kwenye gari la polisi kwa hatua zaidi za kisheria. Akizungumza wakati wa oparesheni hiyo Matiro ambaye alikuwa ameambatana na maafisa mbalimbali na askari polisi alisema hataki kuona miti iliyopandwa kupitia kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa Septemba 23,2017 yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ inakufa kwa uzembe kwani walikubaliana kil...

Manchester united win 2-1 over chelsea

Image
It was an excellent weekend for Manchester United. Jose Mourinho's side beat Chelsea 2-1 at Old Trafford thanks to goals from Romelu Lukaku and Jesse Lingard. Lukaku also set up the winner and was deservedly Man of the Match against his former club, while Nemanja Matic also came back to haunt Chelsea with an excellent second half display. "He played fantastically well," Mourinho said of Lukaku. "He had, in my opinion, the same start as the team. "But then he went together with the team, the team was improving, improving, improving and he probably finished the game, for people [watching] at home, with the image of that incredible sprint that could have handed him a goal but handed an image of a team that gave absolutely everything to try and win an important match for us."